Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae akamwambia kwa ukali "Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo zako na…….. Kabla hajamalizia sentensi simu ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake. Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku jamaa anasikia "Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni 20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio. Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama ana mradi mwingine nimpe hela kidogo".Baada ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa akamuuliza,"eeenhee!!! ulikuwa unasema umenichoka nikusanye nguo zangu halafu iweje? Jamaa kwa upole akajibu "Nilikuwa nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue".