Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/mobile/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.

Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.

Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.

Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: โ€œSasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.โ€

Akajibu: โ€œMimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.โ€
.
.
.

FUNZO:

Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.

Meno huungโ€™ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.

1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.

2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.

3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.

Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.

Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.

*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.

Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima katika Familia: Kuweka Mipaka na Kuheshimiana

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima katika Familia: Kuweka Mipaka na Kuheshimiana

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima katika Familia: Kuweka Mipaka na Kuheshimiana

Kati... Read More

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Ushawishi katika Mahusiano

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Ushawishi katika Mahusiano

Mahusiano ni kitu muhimu sana kwa kila mtu, na kila mmoja wetu anahitaji uhusiano ambao ni imara,... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Elimu na Kukuza Ujuzi katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Elimu na Kukuza Ujuzi katika Familia

Elimu ni kitu muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku. Kupitia elimu tunapata maarifa na ujuzi a... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kujenga na Watoto: Kusikiliza na Kuelewa

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kujenga na Watoto: Kusikiliza na Kuelewa

Habari ndugu yangu! Umeamua kuchagua njia sahihi ya kuwa na mazungumzo ya kujenga na watoto wako.... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maamuzi muhimu ya kifamilia

Kuwajibika na kufanya maamuzi muhimu ya kifamilia ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kudumu. Hapa kuna ... Read More
Kuweka Kipaumbele cha Kuishi kwa Uwiano na Kustawisha Maendeleo ya Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kuishi kwa Uwiano na Kustawisha Maendeleo ya Familia

Kuweka kipaumbele cha kuishi kwa uwiano na kustawisha maendeleo ya familia ni jambo muhimu sana k... Read More

Jinsi ya Kupanga Tarehe ya Kipekee na Msichana Wako

Jinsi ya Kupanga Tarehe ya Kipekee na Msichana Wako

Jinsi ya Kupanga Tarehe ya Kipekee na Msichana Wako

Kupanga tarehe ya kipekee na msichana ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana katika Mazoezi na Huduma ya Kimwili na mke wako

Jinsi ya Kusaidiana katika Mazoezi na Huduma ya Kimwili na mke wako

Kusaidiana katika mazoezi na huduma ya kimwili ni njia nzuri ya kujenga afya na ustawi pamoja na mke... Read More
Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwamb... Read More

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Hakuna kitu kizuri kama ... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu tena kwenye blogu yetu ya mapenzi. Leo tutaangazia swali linaloulizwa mara kwa mara kuhusu... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana kuhusu changamoto na matatizo ya kifedha na mpenzi wako

Jinsi ya Kuwasiliana kuhusu changamoto na matatizo ya kifedha na mpenzi wako

Kuwasiliana kuhusu changamoto na matatizo ya kifedha na mpenzi wako ni muhimu katika kudumisha uamin... Read More
๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About