Namna ya kuvaa vizuri kwa mwanamme upendeze na kuwa mtanashati
Date: April 18, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Nimeona leo nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha.
1.Epuka kuvaa marangirangi
Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi, rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba.
2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu
Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira, sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe
3. Masharti ya kuchomekea
-Marufuku kuvaa oversize/undersize
-Usivae mlegezo
-Hakikisha singlet haionekani
-Usivae mkanda mrefu
-Usivae makubanzi/sandals
4. Kama umevaa pensi /kaptula.
-Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
-Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
-Haipendezi kuchemekea
5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi
Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule
6. Hakikisha una suruali nyeusi
Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi.
7. Saa
-Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote
-Kama umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic.
8. Miwani
Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama madenge na macho kama bundi kisha unapiga miwani ndogo ya njano,ni
9. Vaa kofia za kijanja
Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na kuvaa dera tu
10. Mkanda
-Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka kiunoni
-Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula
-Jitahidi mkumatch rangi ya mkanda na viatu kama umevaa nguo za kuchomekea
-Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako
11.Tupia cheni za ukweli
Mikufu ya kiume pia huongeza mvuto
-Kama umevaa nguo za kuchomekea au suti itapendeza ukivaa cheni ndogo ambayo haitokezi nje ya shati
-Kama umepiga pamba za kishua mfano T.shirt na jeans hapa tupia cheni kubwa lakini hata cheni ndogo zinakubali
12.Uvaaji wa Tai
-Vaa kulingana na urefu wako
-Kama wewe mwembamba inapendeza kuvaa tie nyembamba
-Jitahidi kumatch tie na rangi ya shirt/suruali
-Hakikisha tie yako imefungwa vizuri shingoni
13.T.shirt na Jeans
Wanaume wajanja wa mjini hupenda kupiga t shirt na jeans na chini kutupia raba Kaliโฆ..Vazi hili lina mvuto wa aina yake hasa likivaliwa kitaani na sehemu za mitoko kama vile kwenye Club za starehe.
14. Vaa viatu kijanja
Hapa pia Kuna changamoto
-Usivaa suruali ya kitambaa na Raba
-Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi
-Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na rangi ya viatu
-Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali โฆ.ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X yenye matairi ya Fuso !!!
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni ( Chunusi ). Kuwa na chunus...
Read More
Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwez...
Read More
Mwanamke unywele hasa ukiwa nao, hii ni kauli upya ambayo Muungwana blog inakupa siku ya leo. Mio...
Read More
Makovu sio kidonda naomba hili uelewe, ila makovu ni alama ya majeraha ambayo yamebaki kwenye ngo...
Read More
Ngozi nyeusi katika magoti na nyuma ya mikono hutokana na mkusanyiko wa cells zilizokufa, na hata...
Read More
KUMEKUWA na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya ...
Read More
Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu ...
Read More
Wakati mwingine ili uweze kuboresha mwonekanao wa ngozi yako si lazima utumie makemikali yenye viamb...
Read More
Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina...
Read More
Wengi wetu tunashindwa kutofautisha mavazi ya sehemu husika mfano Ofisini, michezoni, na yale ya ...
Read More
Kuwa na nywele zenye afya nzuri ni muhimu kwa wote bila kujali jinsi, hali hii husababisha wengi ...
Read More
Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi ...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!