Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Kwa nini mara nyingine mimba inatungwa kwenye mrija wa kupitisha mayai badala ya kwenye tumbo la uzazi?

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Mara nyingi utunguaji mimba nje ya mfuko wa uzazi hutokea kwa sababu ya maradhi kwenye via vya uzazi. Maradhi hayo huharibu mirija ya kupitisha mayai. Uharibifu huo hufanya yai lisiweze kufika kwenye mfuko wa mimba na mara nyingi unasababishwa na magonjwa ya zinaa. Kama mwanamke alikuwa na magonjwa ya zinaa uwezekano wa kutunga mimba kwenye mrija wa kupitia mayai unaongezeka.
Ikiwa unafikiri una mimba au iwapo una maumivu chini ya tumbo, unashauriwa uende kliniki kwa ajili ya uchunguzi.
Yai lililorutubishwa linapokaa kwenye mrija wa kupitisha mayai tunasema mimba i imetungwa nje ya mji wa mimba”ectopic pregnancy”. Kwa maana hiyo basi,, ukuta mwembamba wa mrija utashindwa kutanuka kikamilifu i ili kubeba mimba i inayokua. Mrija hupasuka na damu kutoka. Ikitokea hali hii , lazima mwanamke aende hospitali kwa ajili ya kupasuliwa na pengine kuongezwa damu.

AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 0

Please log in or register to comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts! πŸ“

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About