Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/mobile/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au natureโ€™s call.

Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili. Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wanafanya.

Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa. Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili (Receptors) vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.

Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani, automatic, kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha Ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa Ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo. Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika kuvumilia kidogo ili afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena na kujikuta muda mdogo tuโ€ฆ.mtu tayari kaloanisha nguo yake.

Mpenzi msomaji, mtu kujibana na kupuuzia kwenda kukojoa husababisha uwezo wa kibofu cha mkojo kujitawala (control) upotee. Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi misuli maalumu ya kubana mkojo (sphincter) itashindwa kuachia na matokeo yake mtu ataendelea kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu ambacho ni hatari kwa afya yake. Endapo mkojo huu utashindwa kutoka, utatengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection). Magonjwa ya kibofu cha mkojo ni pamoja na U.T.I (Urinary Tract Infections), pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na mchafuko wa damu, bacteremia.

Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu, yawezekana alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila akinywa maji au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka bombani, basi atahisi kwenda kukojoa.

Mpenzi msomaji, ni vyema tukawa wasikivu pale mtu unapobanwa na mkojo, hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo, usisite kuonana na wataalamu wa afya.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kutibu chunusi kwa ute mweupe wa yai

Kutibu chunusi kwa ute mweupe wa yai

Hii inaweza kuchukuliwa kama njia rahisi na isiyo na gharma katika kutibu chunusi. Kwa mjibu wa ... Read More

Madhara ya kunywa soda

Madhara ya kunywa soda

Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dum... Read More

Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula

Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula

Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyaku... Read More

Vyakula vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Vyakula vinavyofaa kuliwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Vyakula vinavyofaa kuliwa wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaan... Read More

Faida za mnyonyo na mazao yake

Faida za mnyonyo na mazao yake

Nyonyo Mbarika (Castor)
Mnyony(KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka(KiRusi) ni mmea wa jamii ... Read More

Faida za kula tunda la apple (tufaa)

Faida za kula tunda la apple (tufaa)

Tunda asili yake ni sehemu za Mashariki mwa Europe na pia Magharibi mwa Asia, na tunda hili linaj... Read More

Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Chunusi ni nini?