Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Mapishi ya Pilau Ya Mchicha

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

VIPIMO

Mchele - 3 Vikombe

Mchicha

Mafuta - 1/2 kikombe

Vitunguu maji - 2 vikubwa

Nyanya - 1

Viazi - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 3 vijiko vya supu

Vidonge vya supu (Stock cubes) - 3

Jiyrah (cummin powder) - 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Hiliki ya unga - 1/2 kijiko cha chai

Mdalasini - 1 kijiti

Maji (inategemea mchele) - 5 vikombe

Chumvi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Osha na roweka mchele.

2. Osha mchicha, chuja maji na katakata.

3. Katakata vitunguu maji, nyanya.

4. Menya na kata viazi vipande ukaange pekee vitoe weka kando.

5. Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi.

6. Tia thomu, bizari zote, kaanga kidogo kisha nyanya.

7. Tia mchicha kaanga kidogo kisha tia mchele, maji na vidonge vya supu, chumvi.

8. Koroga kidogo kisha tia viazi ulivyovikaanga, funika na acha uchemke kidogo katika moto mdogo mdogo.

9. Kabla ya kukauka maji, mimina katika chombo cha kupikia ndani ya oven (oven proof) au katika treya za foil, funika vizuri na upike ndani ya oven moto wa 400ΒΊ kwa dakika 15-20 upikike hadi uive.

10. Ukishaiva epua na tayari kuliwa na kitoweo chochote upendacho.

AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 0

Please log in or register to comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts! πŸ“

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About