Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ

Jinsi ya kutengeneza Biriani Ya Nyama Ya Ng'ombe

โ€ข
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image

Mahitaji

Nyama - 2 Ratili (LB)

Chumvi - kiasi

Mafuta - 1 Kikombe

Samli - ยฝ Kikombe

Kitungu (Kata virefu virefu) - 3 Vikubwa

Nyanya (kata vipande) - 2

Nyanya kopo - 1 Kijiko cha chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chakula

Tangawazi - 1 Kijiko cha chakula

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai

Pilipili ya unga nyekundu - ยฝ Kijiko cha chai

Kotmiri iliyokatwa - 2 Vijiko vya chakula

Viazi - 6

Gram masala - 1 Kijiko cha chai

Mtindi - ยผ Kikombe cha chai

Namna Ya kutaarisha Na Kupika

1. Kwenya karai au (sufuria) mimina mafuta na samli. Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.
2. Kaanga viazi na viweke pembeni.
3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi, na pilipili ya unga. Chemsha mpaka iive.
4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, gram masala, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ยผ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ยผ saa, epua weka pembeni.

Vipimo Vya Wali

Mchele - 5 Magi (Kikombe kikubwa)
Hiliki nzima - 4
Mdalasini mzima - 1
Zafarani - ยฝ kijiko cha chai
Rangi ya biriani - ยผ Kijiko cha
Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu - ยฝ Kikombe
Chumvi - kiasi
Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ยผ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.

Namna Ya Kutaarisha

Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.
Tia hiliki na mdalasini.
Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.
Unamimina tena ule mchele ยฝ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo, halafu unamimina
mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.
Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka
moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.
Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama

AckySHINE Solutions
โœจ Join AckySHINE for more features! โœจ

Comments 0

Please log in or register to comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts! ๐Ÿ“

๐Ÿ”— Related Posts

๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About