MAHITAJI
Unga - 3 Vikombe vya chai
Baking powder - 1 ยฝ Vijiko vya chai
Sukari - 1 Kikombe cha chai
Siagi - 1 Kikombe cha chai
Mayai - 2
Maji - kiasi ya kuchanganyia
Tende - 1 Kikombe
ufuta - ยผkikombe
MAPISHI
- Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli
- Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.
- Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.
- Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.
- Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande.
- Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350ยฐF kwa muda wa nusu saa takriban.
- Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!