Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.
Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.
Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.
Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.
Wakaingia msituni kila mtu njia yake.
β¦ Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.
Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini⦠alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.
Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, βVipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?β
Mkenya akamjibu: βMkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!β
Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina. Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa. Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao. Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana. Wakaingia msituni kila mtu njia yake. β¦ Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa. Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala niniβ¦ alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa. Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, βVipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?β Mkenya akamjibu: βMkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!β
π¬
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
236 comment(s)
π Login required to comment or reply
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Kula lishe boraChakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.Punβ¦
Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kilaβ¦
Nini maana ya Kwaresima? Kwa Kilatini na Kiitaliano neno Kwaresima lilimaanisha β40β yaani siku 40 za kufunga za wiki kati ya Jumatano ya Majivu hadi β¦
Mapenzi ni matamu napia yana raha, wewe hauni ishi hamu,siku zote wanipa raha, wewe kwangu ni mtumuhimu, unaeng'aa moyoni mwangu kama nyota ya jaha."Nβ¦
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate