Usipite bila kusoma kisa hiki cha kusisimua

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2016-01-21 15:38:00πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~2 min read
πŸ“„ PDF

Siku moja jioni katika mji flani, kulikuwa na basi likisafiri kutoka mji huo kuelekea mji mwingine. Lilikuwa ni basi kubwa na limejaa abiria. Wakati wakiendelea na safari, ghafla, mvua kubwa iliyoambatana na radi ikaanza kunyesha. Dereva hakuogopa, wala abiria, wakaendelea na safari. Mara wakati wanaenda, radi ikaanza kufuatilia gari. Kila wakienda, radi inapiga karibu na basi kana kwamba inalifuata basi. Likisimama, radi inapiga pembezoni mwa basi.

Dereva kuona hivyo, akasimamisha gari mita 5 kutoka kwenye mti… Akawaambia abiria, "Humu ndani ya basi, kuna mtu ambaye leo ni siku yake ya kufa, tena kufa kwa radi. Ili tusife wote, nataka kila abiria ashuke akaguse mti ili anayepigwa na radi, apigwe wengine wasife kwa ajili yake. "Abiria wakitetemeka, wakaanza kushuka mmoja mmoja. Unaenda unagusa mti , kisha unarudi kwenye basi. Abiria wote pamoja na dereva mmoja mmoja, wakaenda, wakagusa mti na kurudi bila dhara lolote! Akawa kabaki abiria mmoja tu, ambaye alikuwa hajagusa mti. Abiria wote kwa macho ya hasira wakamwambia akaguse mti. Akawa anaogopa kufa. Akagoma. Wakamlazimisha kwa nguvu sana na kumtoa nje……. …….. Yule abiria akiwa amefumba macho, akaenda akagusa mti. Hamadi bin Vuu! Radi kali sana ikalipiga basi, abiria na wote waliokuwamo, wakafa palepale. Kumbe uwepo wake ndio ulikuwa unazuia abiria wengine wasidhurike na radi.

MAFUNZO

1. Unapofanikiwa, huwezi jua uwepo wa nani umefanikisha mafanikio yako, usichukue sifa zote peke yako. Wapatie na wengine bila kumsahau MUNGU.
2. Unaweza kujiona huna thamani sehemu ulipo, iwe kwenye kundi la WhatsApp, darasani, kazini, kwenye basi, barabarani bila kujua kama uwepo wako ni wa muhimu sana kwa ustawi wa wengine.
3. Usimtenge wala kumnyanyasa mtu au jirani yako, huwezi jua uwepo wake ni kwa ajili gani.

πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
J
Josephine Nekesa2016-11-12 21:06:10
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
A
Anna Malela2016-09-29 12:41:26
Nakuombea πŸ™
J
Janet Mwikali2016-07-02 21:39:39
Sifa kwa Bwana!
P
Paul Ndomba2016-06-16 16:32:40
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
L
Linda Karimi2015-11-29 11:40:17
Mwamini katika mpango wake.
M
Monica Lissu2015-10-16 16:23:01
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
N
Nancy Akumu2015-10-13 06:44:49
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
J
John Lissu2015-09-13 15:48:28
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
N
Nancy Kawawa2015-08-16 04:56:26
Tembea kwa imani, si kwa kuona
S
Susan Wangari2015-06-19 14:05:52
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu