Mambo 7 ya kubadili katika maisha ili ubadilike

โœ๏ธ DIN - Melkisedeck Leon Shine๐Ÿ“… 2017-01-17 17:04:00๐Ÿ’ฌ 50 commentsโฑ๏ธ ~2 min read
๐Ÿ“„ PDF

1. Huwezi kubadili namna watu walivyokutendea mpaka ubadili namna unavyowatendea.โ€‹

Matayo 7:12;
"Basi yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii."

โ€‹2. Huwezi kubadili tabia mpaka ubadili marafiki.โ€‹

1Wakorintho 15:33
"Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema."

โ€‹3. Huwezi kubadili ulichovuna mpaka ubadili ulichokipanda.โ€‹

Wagalatia 6:7;
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna."

โ€‹4. Huwezi kubadili mwelekeo wa maisha yako mpaka ubadili dereva.โ€‹

Kutoka 23:1-3;
"Msivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. Usiwafuate walio wengi katika kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotosha hukumu; wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake".

Maisha yako yaweza ongozwa na mkumbo wa watu au โ€‹MSIMAMOโ€‹ wako โ€‹BINAFSIโ€‹ kwa โ€‹UNACHOKIAMINI.โ€‹

โ€‹5. Huwezi kubadili hali yako ya kifedha mpaka ubadili tabia yako ya kifedha.โ€‹

Mithali 21:17;
Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; yeyote apendaye mvinyo, kula na manukato hatakuwa tajiri."

โ€‹Mtindo wa maisha ya ufukara ndiyo busara kwa wengi.โ€‹

โ€‹6. Huwezi kunibadili mpaka ujibadili mwenyewe.โ€‹

Matayo 7:3-5.
"Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huioni? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako."

โ€‹7. Huwezi kubadili mtazamo wako wa kifikra mpaka ubadilipo usikiacho.โ€‹

Mithali 23:7;
"Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia haya kula, kunywa; lakini moyo wake hauwi pamoja nawe."

โ€‹(Waache wenye Hekima wasikilize na kuongeza ufahamu wao.)โ€‹

Huyo anayesikiliza, huashiria na kuamua kile anachojifunza.

Kile unachojifunza, huashiria uelewa ulio nao kichwani mwako.

Uelewa ulionao kichwani mwako, huashiria maamuzi yako.

Na maamuzi yako, huashiria โ€‹mwelekeo wa maisha yako.โ€‹

๐Ÿ’ฌ

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
๐Ÿ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
M
Mercy Atieno2017-05-24 03:03:00
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
G
George Ndungu2017-04-22 03:52:33
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
B
Benjamin Kibicho2017-01-29 01:02:35
Mwamini Bwana; anajua njia
J
Janet Sumaye2017-01-24 19:17:20
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
F
Frank Sokoine2016-08-06 01:10:02
Rehema zake hudumu milele
J
Janet Mbithe2016-04-25 14:26:12
Dumu katika Bwana.
P
Peter Mugendi2016-04-24 20:52:54
Mungu akubariki!
G
Grace Mushi2016-03-09 08:29:47
Wakati wa Mungu ni kamilifu
L
Lydia Wanyama2015-10-11 17:09:24
Endelea kuwa na imani!
G
Grace Minja2015-05-25 12:29:00
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni