Kilichowapata Watu 8 waliowahi kumdhihaki Mungu

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2015-01-17 17:18:00πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~3 min read
πŸ“„ PDF

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la #American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya #Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata #MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la #Rio #De #Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema #Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, Mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata #Mungu hawezi kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa Mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa Mama, huyo #Mungu labda akae kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya…kibaya na kibaya kama #Biblia"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na #Bill #Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simhitaji #Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.

#share Ujumbe huu Kwa Ndugu na jamaa,ujumbe huu utawasidia kumuheshimu Mungu na kumtii.

Mungu ni pendo

πŸ’¬

Discussion

Share a thoughtful comment or reply. Content is escaped before display.

50 comment(s)
G
Grace Njuguna2017-03-17 06:59:02
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
L
Lucy Mushi2017-03-02 04:45:08
Dumu katika Bwana.
J
Janet Mwikali2016-11-29 00:03:59
Rehema hushinda hukumu
E
Edward Chepkoech2016-08-01 15:01:32
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
S
Samuel Were2016-07-01 20:45:23
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
J
Jane Muthui2016-03-11 20:59:05
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
G
Grace Njuguna2015-12-26 08:55:17
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
E
Elizabeth Malima2015-09-28 15:32:08
Baraka kwako na familia yako.
K
Kevin Maina2015-08-02 01:12:10
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
C
Carol Nyakio2015-05-01 02:58:23
Katika imani, yote yanawezekana