Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Inatupasa kusali kila siku bila kukata tama kwa ibada, kwa matumaini na kwa saburi. Kama mfano Yesu Alitufundisha sala ya Baba yetu.
Yatupasa kuwaombea wengine, watu wote wenye shida wakosefu na hata maadui zetu, vilevile tumtolee Mungu shukrani kila wakati na hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu.
Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu.
Sababu za kusali
1. Kumuabudu Mungu
2. Kumshukuru Mungu
3. Kuomba Neema na Baraka kwa ajili yetu na wenzetu
4. Kuomba msamaha
Namna za sala
1. Sala ya sauti :Β Sala asaliyo mtu au kikundi kwa kutumia maneno
2. Sala ya fikra :Β Sala asaliyo mtu akiwa peke yake au na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu.
3. Sala ya Taamuli:Β Kumtazama tuu Mungu kwa upendo Mkubwa Moyoni.
Nyakati zote zinafaa kwa sala hasa
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi
Vyanzo vya sala za Kikristo
1. Neno la Mungu
2. Liturujia ya Kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku
Aidha Roho Mtakatifu ndiye mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo akitufundisha kusali na kusali ndani mwetu.
Sala Muhimu kwa Mkristo
Sala kubwa ya kanisa ni Misa Takatifu na sala Bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu.
Sala nyingine Muhimu kwa Mkristu ni:
1. Baraka ya Sakramenti kuu
2. Andamo la Ekaristi
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari takatifu
6. Novena
Mtu anaweza kusali popote lakini kanisani ndio mahali rasmi pa sala, Aidha familia ni shule ya kwanza ya sala ambapo mtu hujifunza na kujizoesha kusali anapokua katika familia.
Changamoto na majaribu wakati wa kusali
1. Mtawanyiko wa mawazo
2. Ukavu wa Moyo
3. Uvivu na uregevu
Faida ya Sala
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili tushinde vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema
NenoΒ AminaΒ katika sala linamaanaΒ βNa iwe hivyoβ.Β Na nenoΒ AeluyaΒ maana yake niΒ Msifuni Mungu.
Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Inatupasa kusali kila siku bila kukata tama kwa ibada, kwa matumaini na kwa saburi. Kama mfano Yesu Alitufundisha sala ya Baba yetu.Yatupasa kuwaombea wengine, watu wote wenye shida wakosefu na hata maadui zetu, vilevile tumtolee Mungu shukrani kila wakati na hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu.Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu.Sababu za kusali1. Kumuabudu Mungu2. Kumshukuru Mungu3. Kuomba Neema na Baraka kwa ajili yetu na wenzetu4. Kuomba msamahaNamna za sala1. Sala ya sauti : Sala asaliyo mtu au kikundi kwa kutumia maneno2. Sala ya fikra : Sala asaliyo mtu akiwa peke yake au na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu.3. Sala ya Taamuli: Kumtazama tuu Mungu kwa upendo Mkubwa Moyoni.Nyakati zote zinafaa kwa sala hasa1. Asubuhi na jioni2. Kabla na baada ya kula3. Kila dominika4. Sikukuu za amri5. Kabla na baada ya kazi6. Katika kishawishiVyanzo vya sala za Kikristo1. Neno la Mungu2. Liturujia ya Kanisa3. Fadhila za Kimungu4. Matukio ya kila sikuAidha Roho Mtakatifu ndiye mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo akitufundisha kusali na kusali ndani mwetu.Sala Muhimu kwa MkristoSala kubwa ya kanisa ni Misa Takatifu na sala Bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu.Sala nyingine Muhimu kwa Mkristu ni:1. Baraka ya Sakramenti kuu2. Andamo la Ekaristi3. Litania Takatifu4. Njia ya Msalaba5. Rozari takatifu6. NovenaMtu anaweza kusali popote lakini kanisani ndio mahali rasmi pa sala, Aidha familia ni shule ya kwanza ya sala ambapo mtu hujifunza na kujizoesha kusali anapokua katika familia.Changamoto na majaribu wakati wa kusali1. Mtawanyiko wa mawazo2. Ukavu wa Moyo3. Uvivu na uregevuFaida ya Sala1. Zinaleta neema nyingi2. Zinatuimarisha ili tushinde vishawishi na dhambi3. Zinatuunganisha na Mungu4. Zinatudumisha katika kutenda memaNeno Amina katika sala linamaana βNa iwe hivyoβ. Na neno Aeluya maana yake ni Msifuni Mungu.
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate