Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2016-01-17 16:59:00πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~2 min read
πŸ“„ PDF
Angalizo; Tunapoongelea kuhusu pombe sio kwamba tunahamasisha kutumia pombe bali tuelewe kile tunachofanya kwa mapenzi ya Mungu! pombe haikukataliwa ila itumike kwa kiasi. Mhubiri 9:7 Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako. Tito 2:3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; 1Timotheo 5:21,23 "21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda. 23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara. Yoshua Bin Sira 31:25-29 "25 Usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa pombe, maana imewaangamiza wengi. 26 Tanuru hupima ugumu wa chuma, na pombe hupima mioyo katika shindano la wenye kiburi. 27 Pombe ni kama uhai kwa mtu akinywa kwa kiasi, Maisha yafaa nini bila pombe? Imeumbwa iwafurahishe watu. 28 Kunywa pombe kwa wakati wake na kwa kiasi, kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni. 29 Lakini kunywa pombe kupita kiasi, kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha." Wakolosai 2:16-18a "kwa hiyo basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu VYAKULA au VINYWAJI, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au sabato. 17 mambo ya namna hiyo ni kivuli cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye kristo. 18 msikubali kuhukumiwa na mtu anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee…." Luka 7:31-35 "31 Yesu akaendelea kusema, "Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani? 32 Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine: 'Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza! Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!' 33 Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: 'Amepagawa na pepo!' 34 Naye mwana wa Mtu amekuja anakula na kunywa, nanyi mkasema: 'Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi!' 35 Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote wale wanaoikubali." #Note; mvyinyo itumike kwa kiasi, kama huwezi kutumia kwa kiasi, ni afadhali kuacha kabisa.
πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
C
Charles Mboje2020-02-25 01:39:09
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
C
Catherine Naliaka2019-12-25 21:04:43
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
D
Diana Mallya2019-12-15 08:05:48
Mwamini katika mpango wake.
V
Victor Malima2019-11-14 01:43:49
Endelea kuwa na imani!
G
Grace Mligo2019-07-30 19:13:08
Kwa Mungu, yote yanawezekana
V
Victor Sokoine2019-05-02 05:47:55
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
A
Anna Kibwana2019-04-21 17:54:33
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
P
Peter Mbise2019-02-20 15:17:57
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
D
Dorothy Nkya2019-02-05 08:02:18
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
G
Grace Njuguna2018-11-12 10:20:48
Sifa kwa Bwana!
P
Patrick Kidata2018-08-07 16:16:49
Katika imani, yote yanawezekana
M
Mary Njeri2018-07-05 18:52:17
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
R
Ruth Wanjiku2018-05-18 13:03:42
Imani inaweza kusogeza milima
P
Peter Mwambui2017-12-20 14:47:56
Neema na amani iwe nawe.
E
Elizabeth Mtei2017-11-13 19:37:41
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
P
Patrick Akech2017-07-26 09:49:08
Neema ya Mungu inatosha kwako
J
Joyce Nkya2017-06-26 19:43:40
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
H
Henry Mollel2017-03-17 09:18:23
Mungu akubariki!
M
Mary Njeri2017-02-19 17:40:55
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
M
Margaret Anyango2016-12-24 15:57:53
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi