Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako.
Updated at: 2024-05-27 07:14:10 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake, utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako. Ee Mlinzi amini wa Jamaa Takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristo, ee Baba uliyetupenda mno, utuepusha na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji,utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwokoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi, ulikinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote, mtunze daima kila mmoja wetu, tupate mfano wako, tusaidie kwa msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupokelewa mbinguni makao ya raha milele. Amina
SALA KWA MT. YOSEFU KWA AJILI YA KULIOMBEA KANISA LA MAHUJAJI
Ee Mtukufu Mt. Yosefu, ulichaguliwa na Mungu kuwa Baba Mlishi wa Yesu, mchumba safi kabisa wa Maria Bikira Milele, na mkubwa wa Familia Takatifu. Umechaguliwa na Mwakilishi wa Kristu kama Msimamizi wa kimbingu na mlinzi wa Kanisa alilolianzisha Kristu. Ndiyo maana ninakuomba kwa matumaini makuu usaidizi wako wenye nguvu kwa ajili ya Kanisa zima duniani.
Updated at: 2024-05-27 07:14:02 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Ee Mtukufu Mt. Yosefu, ulichaguliwa na Mungu kuwa Baba Mlishi wa Yesu, mchumba safi kabisa wa Maria Bikira Milele, na mkubwa wa Familia Takatifu. Umechaguliwa na Mwakilishi wa Kristu kama Msimamizi wa kimbingu na mlinzi wa Kanisa alilolianzisha Kristu. Ndiyo maana ninakuomba kwa matumaini makuu usaidizi wako wenye nguvu kwa ajili ya Kanisa zima duniani.
Mlinde kwa namna ya pekee, kwa upendo wa kikweli wa ki-baba, Baba Mtakatifu na Maaskofu wote na Mapadre wenye ushirika na Kiti cha Petro. Uwe mlinzi wao wote wanaotumikia wokovu wa wanadamu kati ya majaribu na mahangaiko ya maisha haya, na utujalie kwamba watu wote wa dunia hii wamfuate Kristu na Kanisa alilolianzisha.
Mpendwa Mtakatifu Yosefu, ukubali majitoleo ya nafsi yangu ambayo sasa ninafanya. Ninajiweka wakfu kwako kwa ajili ya utumishi wako, ili daima wewe uwe baba yangu, mlinzi wangu, na kiongozi wangu katika njia ya wokovu. Unijalie usafi mkuu wa moyo na matamanio makuu ya maisha ya kiroho. Unijalie ili matendo yangu yote, kwa mfano wako, yawe kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu, pamoja na Moyo wa kimungu wa Yesu, moyo safi wa Maria, na moyo wako wa ki-baba. Uniombee, nami nishiriki kifo chako cha furaha na kitakatifu. Amina.
Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo na mafungu 7 yaani mateso 7 yenye Salamu Maria saba kwa kila teso.
TESO LA KWANZA
Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga. Tuombe neema ya kuvumilia mateso. Mama wa mateso utuombee.
Updated at: 2024-05-27 07:14:15 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo na mafungu 7 yaani mateso 7 yenye Salamu Maria saba kwa kila teso.
TESO LA KWANZA
Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga. Tuombe neema ya kuvumilia mateso. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba …… Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA PILI
Maria na Yosefu walikimbilia Misri usiku ili kumficha Mtoto Yesu asiuawe na Herodi. Tuombe neema ili miili yetu iwe kimbilio lake Yesu. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba …… Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA TATU
Mama Maria aliona uchungu sana Mtoto Yesu alipopotea kwa siku tatu. Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba …… Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA NNE
Mama Maria aliona uchungu sana alipokutana na Mwanae Yesu katika njia ya Msalaba. Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba …… Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA TANO
Mama Maria aliona uchungu sana alipomwona Mwanae Yesu akisulibiwa Msalabani. Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Maria. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba …… Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA SITA
Mama Maria aliona uchungu sana alipopakata maiti ya Mwanae Yesu baada ya kushushwa Msalabani. Tuombe neema ya kutotenda dhambi. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba …… Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA SABA
Mama Maria aliona uchungu sana aliporudi nyumbani baada ya kumzika Mwanae Yesu Tuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba …… Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.