Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Updated at: 2024-05-25 15:36:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
SMS ya mapenzi kutakia maisha marefu siku ya kuzaliwa au birthday
Updated at: 2024-05-25 15:26:21 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi, pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi, nakupenda la azizi.
SMS ya ujumbe wa kimahaba wa kifumbo kwa mpenzi wako
Updated at: 2024-05-25 15:25:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila mtu anataka kuwa jua linalong’arisha maisha yako, lakini ni afadhali niwe mwezi, ili nikuangazie wakati wa giza ambapo jua limechwea na haliangazi tena.
Updated at: 2024-05-25 15:26:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Swt ulivyoumbika wengi wanateseka juu yako ,najua wanakusumbua ni vema usiwakubalie, ukweli umebarikiwa uzuri umeshushiwa na dhati ya penzi umetunukiwa nakupenda
Updated at: 2024-05-25 15:27:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Updated at: 2024-05-25 15:36:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Raha ya ndege kichaka si tunduni asilani, Raha ya Ndege ujumbe nakupa mpelekee mwandani iwapo hukumkuta msubiri mlangoni, Usije ukaondoka hakuchinji asilani, Mwambie namkumbuka hatoki mwangu moyoni. ucku mwema
SMS ya kumtumia mpenzi wako kujivunia kuwa na yeye
Updated at: 2024-05-25 15:24:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Furaha yangu ni kuwa nawe kwani u zaid ya mboni yangu,najisifu kuwa nawe maishani mwangu naamini itatokea kutokuwa mbali nawe mpz wangu,unisahaulishe machungu na karaha za huu ulimwengu .nakupenda dia.