Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
*Mdukuzi:* _nikikuuliza swali unaakili ya kujibu?_ *Massai:* _ulisa acha maneno yako._ *Mdukuzi:* _nitajie wanyama kumi wa porini_ *Massai:* _swala watatu na tembo saba_๐๐๐๐๐๐๐๐ฟ
Soma huyu mtoto anachosema sasa, Ndoto za watoto bwana! Kazi ipo!
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
Updated at: 2023-04-29 22:53:28 (1 year ago by Melkisedeck Leon Shine)
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae. MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani? JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo. MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga. MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi. MWAL: Na wewe Nehemiah ?? Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiweโฆโฆ" Akameza mate kisha akaendeleaโฆ. "Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali." MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani?? JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah .!!
Updated at: 2024-05-25 17:54:01 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu, yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka. 2.Manyoya ya mende. 3.Sisimizi Shoga. 4.Mbwa mjane. 5.Kuku aliye single. 6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga 7.Mti wenye ujauzito. 8.Mbavu za Nzi. 9.Nywele za Kiroboto. 10.Mwanya wa Mbu. Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako. Wengine wanasemaga IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Updated at: 2024-05-25 17:05:08 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:
MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono
Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu. Sunday joke