Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 18:12:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday
MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaaliβ¦ mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata 'Laki Moja' ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mweziβ¦?πππππ
Updated at: 2024-05-25 17:15:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna mchepuko nilimtumia nauli jana ili aje,.kwang sasa leo kaniambia eti " nimesahau ile line yenye M-pesa home plz nitumie tena kwa tigo mpenz""!! Me nikajifanya chizi nikatuma Kule kule kwenye voda (aliosema kaacha home) Nikatuma huko message ivi "nikuongezee Sh. Ngapi tena mpenz..!!" Akanjbu "elfu 20,000 tu mpenzi" Mtuhurumie jamani πππ
Updated at: 2024-05-25 17:15:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu? sipendagi ujingaπΆπ» na kitu hela mm!
Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti
Updated at: 2024-05-25 17:10:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dogo kampigia simu baba yake; DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti? DOGO : Lakini baba BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona ntakachofanya. DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda shilingi milioni 3 BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua haraka mwanangu mpenziβ¦
Utajuaje kama unachoangalia ni filamu ya kibongo!!!!
Updated at: 2024-05-25 17:59:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Angalia hivi
-Mlinzi wa Getini lazima awe chizi -Mtu yupo kijijini, maisha magumu ana Wave kichwani. -Kama bosi atakuwa na kampuni basi ni lazima itakuwa ya Clearing and Forwading au ya uuzaji Magari. -Lazima waende Kununua nguo. -Jambazi lazima avae koti lefu jeusi na Miwani. -Mtu akichapwa kofi huangukia kwenye kochi ama kitandani. -Actress huwa hawapiki hata chai. -Kwa mdada akiishi maisha ya kitajiri lazima avae nguo inayoishia mapajani. -Actress even after 5 yeas utakuta staili ya nywele na rangi za kucha ni zile zile. -Anaweka Sumu alafu anaonja kama imekolea. -Movie zote wapenzi huitana Baby.. -Main actor wote ni wafanya biashara na lazima wataongelea mizigo kutoka bandarini. -Wakinywa Soda basi lazima wabakishe.
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
Updated at: 2024-05-25 18:04:32 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitakiβ¦.mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa
Updated at: 2024-05-25 18:11:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hii ndio Bongo
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.
MZEE: Chagua gari unalotaka mpenziβ¦.kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .
BINTI: Mi naitaka hii
MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lakoβ¦
Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.
MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.