ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Thamani ya Kazi ya Upadre

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… February 24, 2020πŸ’¬ 50 comments
πŸ—‚οΈ Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki#Karibu AckySHINE#Katoliki: Kanisa Katoliki#Katoliki: Mapadre#Katoliki: Sakramenti ya Daraja#Katoliki: Watawa wa Kanisa Katoliki#Katoliki: Wito wa Kipekee🌐 Kiswahili
Thamani ya Kazi ya Upadre
UPADRE NI KAZI YA PEKEE YA HEKIMA, UWEZO NA MAPENDO YA UMUNGU WA KRISTU. KAMWE USIMSHAMBULIE PADRE. "Yesu Maria na Yosefu nawapenda, ziokoeni Roho. KUMTETA PADRE [Haya ni maelezo ya Bwana wetu kwa Mutter Vogel.] " Kamwe mtu asimshambulie Padre hata anapokuwa katika makosa badala yake umwombee na fanya toba ili niweze kumpa tena NEEMA.
Ni yeye peke yake anaye niwakilisha mimi hata awe haishi kulingana na mimi. Endapo Padre anaanguka tumnyoshee mkono wa msaada kwa njia ya SALA na sio KUMSHAMBULIA. Ni mimi pekee nitakuwa HAKIMU wake si mwingine ila mimi". "Mtu yeyote anapotamka HUKUMU dhidi ya padre ananihukumu mimi".Β 

Mwanangu kamwe usiruhusu padre ashambuliwe, jitahidi kuwa upande wake na umtetee". Mwanangu kamwe usimhukumu mwungamishi wako bali umwombee sana na tolea KOMUNIO TAKATIFU kwa ajili yake, kila siku ya ALHAMISI kupitia MIKONO au MAMA YANGU MTUKUFU.Β 

Tena kamwe usikubali neno lolote la kumdhalilisha Padre na kusema neno baya dhidi yake (yao), HATA KAMA INGELIKUWA NI KWELI! Kila Padre ni WAKILI wangu na moyo wangu utahuzunika na kusikia uchungu kwa ajili hiyo. Usikiapo HUKUMU dhidi ya Padre, sali SALAMU MARIA. Umwonapo Padre anayeadhimisha MISA TAKATIFU akiwa katika halo isiyostahili, usiongee nae lolote kumhusu yeye bali nieleze mimi tu! Huyo huwa nasimama naye ALTERANI". " Oh waombeeni mapadre wangu ili watamani USAFI NA WEUPE WA ROHO kuliko jambo lolote ili waweze kutolea sadaka TAKATIFU kwa moyo na mikono iliyotakata. Ni ukweli kwamba Misa ni ile ile hata ikiadhimishwa na Padre mwenye hali isiyostahiki lakini NEEMA zinazowashukia watu sio zile zile. [MARIA, MALKIA WA MAPADRE UWAOMBEE.]
βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.