ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Ijue Ishara ya Msalaba

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… February 24, 2020πŸ’¬ 50 comments
πŸ—‚οΈ Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki#Karibu AckySHINE#Katoliki: Imani ya Kanisa Katoliki#Katoliki: Ishara ya Msalaba🌐 Kiswahili
Ijue Ishara ya Msalaba
Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa paji la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka 'Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina'.
Kugusa paji la uso tuna maana kukubali kwa akili, kugusa kifua maana yake ni kupokea na kuupenda msalaba moyoni na kugusa Mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba Msalaba kwa nguvu zetu zote.
Tunafanya njia ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu Mmoja katika Nafsi tatu. Pia Msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu.
Ishara ya Msalaba Juu ya Paji la uso, mdomo na kifua kabla ya injili:
Hii ina maana kwamba Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu Kwa Akili yangu,
Nitalitangaza kishujaa kwa midomo yangu, na Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu Wote.
βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.