ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Tiba mbadala ya chunusi na vipele usoni

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… June 23, 2021πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Dondoo za Urembo na Mitindo#Karibu AckySHINE#SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF#Urembo na Mitindo: Changamoto na Suluhu#Urembo na Mitindo: Wanaume#Urembo na Mitindo: Wanawake#Urembo na Mitindo: Watoto🌐 Kiswahili
Tiba mbadala ya chunusi na vipele usoni

Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni ( Chunusi ). Kuwa na chunusi ni jambo lenye karaha sana, kwani linakufanya upoteze mvuto wako wa asili na hivyo kukukosesha raha.

Zipo njia mbalimbali za asili zinazo weza kutumika kutibu tatizo la chunusi na vipele vya usoni.

Ifuatayo ni miongoni mwa njia bora kabisa na ya uhakika itakayo kusaidia kuondokana na tatizo la Chunusi au vipele kwenye uso.

Komamanga: Maganda Ya Mkomamanga yaliyosagwa, yakichanganywa na habbat sodah ya unga, hutengeneza dawa nzuri ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ( chunusi )

Habbat Soda: Hii ni Habbat Sodah Ya Mbegumbegu. Habbat Sodah iliyosagwa ndio inayo hitajika katika kutengeneza dawa ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ama chunusi.

MAHITAJI:

Habbat Sawdah ya Unga iliyo sagwa.
Nusu kikombe ya maganda ya komamanga yaliyo sagwa.
Nusu kikombe ya siki ya tofaha(apple )

MATAYARISHO NA MATUMIZI

Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, Β½ (nusu)
kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na Β½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple).

Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila siku usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubarid.

βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.