ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… August 11, 2016πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti#Karibu AckySHINE#SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF#Ujasiriamali: Kujitambua na Kuwa na Mafanikio Katika Maisha🌐 Kiswahili
Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana mmoja juu ya Matokeo ya mchezo.

Kwa tabasamu, alijibu "Wako mbele yetu 3-0"!
Nikasema, Kweli!
Mbona huonekani kukata tamaa..?

"Kukata tamaa?
"Yule mvulana aliuliza kwa mshangao…."!?

Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho?

Nina imani na timu yangu na meneja wa timu; Nina hakika tutashinda!

Na kweli, mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele!

Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa, mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; such beautiful faith;

Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi:
"Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?"

Maisha ni kama mchezo.
Kwanini ukate tamaa wakati mwenyezi Mungu ndiye meneja wako?

Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako?

Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa?

Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho.

Lakini maadamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha.

Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.

Usijipulizie kipenga chako cha mwisho we mwenyewe.

JIPE MOYO USIKATE TAMAA!

KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.

KAMWE USIKATE TAMAA.

βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.