Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba ulemavu huu uko tu kwenye
ngozi na siyo kwenye via / mfumo wa uzazi. Kwa maana hiyo
basi; Albino anaweza kuzaa watoto wenye afya nzuri. Pia
wanaweza kuzaa watoto wenye ngozi ya kawaida (blackii) kama
mzazi mwenzie hatakuwa amebeba vinasaba vya ualbino.