Viambaupishi

  1. Mchele (Basmati) - 3 vikombe
  2. Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) - 1 kikombe
  3. Kuku Kidari - 1 LB (ratili)
  4. Mayai - 2 mayai
  5. Vitunguu (vikubwa) - 2 au 3 vidogo
  6. Pili pili manga - 1 kijiko cha chai
  7. Paprika - 1 kijiko cha chai
  8. Chumvi - Kiasi
  9. Mafuta - 1/3 kikombe cha chai
  10. Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
  11. Tangawizi - 1 kijiko cha chai
  12. Kidonge cha supu - 1
  13. Soy sauce - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.

Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)

Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.

Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali

Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.

Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi

Wacha uchemke asilimia 70%

Chuja maji na weka kando

Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu

Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)

Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga

Kisha tia wali changanye vizuri

Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive

Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.