Mungu ni zaidi ya Mzazi na upendo wake ni zaidi ya wa Wazazi

Wakati wazazi waliweza kuaamua kuzaa mtoto tuu, Mungu yeye alikuchagua wewe utungwe mimba na kukulinda ungali tumboni mwa mama yakoβ¦.Wakati wazazi wanasubiri kwa shauku kuona muonekano wako wewe, Mungu anawaweka wajukuu wa wazazi wako/ watoto wako ndani mwakoβ¦. Wakati wazazi wakitafuta chakula kwa ajili yako, Mungu yeye aliwawezesha kukipataβ¦. Wakati wazazi wakingoja kuona unavyoendelea kukua huku wakiwaza hatima ya maisha yako Mungu anakuendeleza na alishapanga maisha yako tangu alipokuchagua uwe mtu ukiwa tumboni mwa mama yakoβ¦. Wazazi wanaweza kukuombea kwa Mungu lakini Mungu ndiye anayeamua akufanyie nini maana Wewe ni wa kwakeβ¦.Wewe na wazazi wako ni watoto wa Baba mmoja ambaye ndiye Mungu.
The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.