1. Nyumba ya kuku iwe safi na kavu muda wote kuzuia ueneaji na kuzaliana kwa vijidudu vya magonjwa 2. Nyumba ya kuku iwe na nafasi za kupitisha hewa ya kutosha ili kuepuka joto na unyevunyevu ambao unachangia uwepo wa magonjwa kwa kuku 3. Hakikisha unaondoa matandazo na takataka zote kwenye banda wakati wote hasa yenye unyevu. 4. Fagia banda na kuhakikisha ni safi wakati wote. Weka matandazo mapya mara kwa mara. 5. Weka sehemu za kutosha kuku kupumzikia. 6. Weka viota vya kutosha. 7. Weka maji sehemu ambayo ni rahisi kusafisha. 8. Hakikisha unaondoa wanyama kama panya na wadudu nyemelezi kwenye sehemu ya malisho ya kuku kwani wao hubeba vimelea vya magonjwa.