GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje? BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu GIRL: Enhee… BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng'ombe napeleka kwa babu yako GIRL: Ooh baby u care.. BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque GIRL: Baby u are awesome… BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula…. GIRL: Enhee…na sisi?? BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives GIRL: Baby I love you BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas….halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani GIRL: Ooh my sweetheart…halafu tukitoka huko?? BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo