πHuruma ya Mungu: Nguvu ya Kufufua na Kurejesha
Huruma ya Mungu ni kama jua ambalo linang'aa kila siku, ikitoa nguvu ya kufufua na kurejesha maisha yetu. Kupitia huruma yake, tunaweza kusimama tena na kuendelea mbele, bila kujali magumu tuliyopitia. Asante Mungu kwa huruma yako isiyo na kikomo!
Open printable article βπKupokea Huruma ya Mungu: Kuishi kwa Shukrani na Ukarimu
Kupokea huruma ya Mungu ni baraka kubwa sana! Ni jambo la kushukuru na kufurahia. Sisi tunapaswa kuishi kwa shukrani na ukarimu kwa sababu tumepokea mengi kutoka kwa Mungu. Ni wakati wa kushiriki neema hii na wengine kwa upendo na wema.
Open printable article βπWakati unapitia magumu usikate tamaa
<p>Kuna Kipindi katika maisha yako unaweza ukapitia mambo Fulani magumu hadi ukaanza kujiuliza,hivi kwa nini yote haya yananitokea?Why Me God?.Na Mimi nimeshawahi kupitia katika hali hii.</p><p>Nilichojifunza ni kuwa hakuna changamoto ya kudumu milele na katika kila kinachoonekana Leo kuwa hakina majibu,ukiamini kuwa inawezekana basi utapata majibu yake.</p>
Open printable article βπUmakini katika kuwaza
Kuwa makini sana na mawazo yako, Yanaweza kukupeleka Mbinguni au motoni.
Kumbuka vile unavyowaza ndivyo utakavyovitenda.
Amua kuwaza mema kutoka ndani ya moyo wako kisha utatenda mema katika maisha yako
Kumbuka Mungu humhukumu mtu kwa mawazo yake maana mawazo ya mtu ndiyo mtu mwenyewe
Tuwaze mema wapenzi ili tuwe wema
Open printable article βπMambo ya kutafakari unapokuwa katika shida kubwa, unapoelekea kukata tamaa
Leo tunatafakari kuhusu wakati wa shida.
Maisha ya mtu yanabadilika wakati wowote kwa namna yoyote yanaweza yakawa mazuri mpaka ukashangaa au yanaweza yasiwe mazuri kama unavyotarajia. Yote hayo ni sehemu ya maisha.
Open printable article βπMungu ni mwenye upendo, Huruma na Rehema hasa kwa Wenye dhambi
Mungu ni mwenye upendo Huruma na Rehema hasa kwa Wenye dhambi.
Mungu yupo tayari kumsikiliza mtu yeyote mwenye dhambi kama ameutambua, amekiri na Kutubu makosa yake.
Mungu akishamsamehe mtu uovu wake anambariki.
Open printable article βπTofauti Wakati Wa Kukomunika Wakati Wa Kupokea Mwili Na Damu ya Yesu Kristo
Wakati wa Kukomunika kila mtu anampokea Yesu kwa namna alivyojiweka tayari. Vile ulivyojiandaa ndivyo na Yesu anakuja kwako.
Open printable article βπTafakari ya leo kuhusu Uaminifu
Uaminifu ni kipimo na kigezo cha Ukamilifu na Utakatifu.
Uaminifu ni ishara ya Upendo na tunda la uvumilivu.
Uaminifu ni alama ya ushirika na Umoja.
Open printable article βπYesu Yupo Karibu na Wewe Unapoanguka Dhambini: Huruma ya Yesu Kristo kwa Mwenye dhambi
Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio wakati ambao Yesu anakua karibu na mtu sana hata kuzidi wakati mwingine wowote.
Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio Yesu anakua karibu zaidi, lakini tatizo ni kwamba huo ni wakati ambao mtu hawezi kutambua uwepo wa Yesu. Neno moja tuu la Matumaini na Upendo wakati huo linaweza kumfungua mtu na kumbadilisha.
Open printable article βπZawadi ya Kipekee kwa Mtu Ambayo Inadumu Milele
Kuna Zawadi moja ya Kipekee ya kumpa mtu ambayo ni Kusali na Kuomwombea Mtu aweze kuingia Mbinguni. Je, ulishawahi kutoa zawadi hii hasa kwa wale unaowapenda? Kila kitu kitabaki hapa duniani na kitapita na kusahauliwa lakini hili halina mwisho
Open printable article βπSafari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu
Fadhila ya Unyenyekevu ni matunda ya Upendo na Uvumilivu kwa hiyo ili kufikia Unyenyekevu yakupasa kuwa na Upendo wa kweli kwa Mungu na Wanadamu huku ukiwa mvumilivu, Mwisho wa yote hayo utapata fadhila ya Unyenyekevu
Open printable article βπSiri za Upendo, Huruma, Rehema na Neema za Mungu
Kadiri Mtu anavyoanguka dhambini na kutubu kweli makosa yake ndivyo na upendo, Huruma, Rehema na Neema za MUNGU zinavyoongezeka katika maisha yake.
Open printable article βπMambo yanayowazuia Waumini na Watumishi wa Mungu Kufikia Ukamilifu na Utakatifu
Leo nimekuandalia Tafakari kuhusu Mambo yanayowazuia Waumini na watumishi wa Mungu Kuishi Kitakatifu na kufikia Ukamilifu. Mambo haya yanaweza yakaonekana sio dhambi au makosa kwa mtu lakini ni vikwazo kwa mtu kufikia Ukamilifu hasa anaposhindwa kuyajua na kuyaepuka. Wengi wanajiona kwamba wako salama lakini kumbe wako katika dhambi.
Open printable article βπSiri ya Kuwa na Amani ya Moyoni au Rohoni
Ili kuwa na Amani ya Moyoni unatakiwa uishi kwa kutimiza wajibu wako wa kiroho na kidunia kama inavyotakiwa na kwa uwezo wako wote, Huku ukiwa na Matumaini ya kua kile unachokifanya kitafanikiwa, ni sahihi na umekifanya vizuri.
Open printable article βπMaana ya kuushinda ulimwengu
Ni kuacha kufuata akili yako na mwili wako huku ukiufuata moyo wako wakati ukijua moyoni mwako Roho Wa Mungu yupo na anafanya kazi.
Open printable article β